KESHA LA ASUBUHI. JUMAMOSI, 22 OCTOBER2016.
WANAOOMBOLEZA WATAFARIJIWA.
Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Mathayo 5:4.
▶ Huzuni inayotajwa hapa ni hali ya kweli ya moyo unaohuzunishwa na dhambi… Mtu anapovutwa kumtazama Yesu akiwa ameinuliwa msalabani, atatambua hali ya dhambi ya binadamu. Ataona kwamba ni dhambi iliyomtesa na kumsulubisha Bwana wa utukufu. Ataona kuwa japo amependwa kwa wema usioelezeka, maisha yake yamekuwa ni onesho lisilokoma la kukosa shukurani na uasi. Amemwacha Rafiki yake mpenzi na kutumia vibaya karama ya mbinguni ambayo ni ya thamani kuliko zote. Ndani yake amemsulubisha upya Mwana wa Mungu na kuchoma upya ule moyo uliovunjika na kutoa damu. Ametenganishwa na Mungu kwa korongo refu la dhambi ambalo ni pana na lenye giza na kina na anaomboleza moyo wake ukiwa umevunjika. Kuomboleza kwa namna hiyo ‘kutafarijiwa.’ Mungu anatudhihirishia hatia yetu ili tupate kumkimbilia Kristo na kupitia kwake tuwekwe huru kutoka kwenye utumwa wa dhambi na kushangilia uhuru wa wana wa Mungu. Katika hali ya majuto ya kweli tunaweza kuja chini ya msalaba na kuibwaga mizigo yetu hapo….
▶Maneno ya Mwokozi yana ujumbe wa faraja kwa wale pia wanaoteseka kutokana na mateso au msiba. Huzuni zetu hazizuki tu kutoka ardhini. Mungu, “moyo wake haupendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Anaporuhusu majaribu na mateso, ni kwa “faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.” Likipokelewa kwa imani, jaribu linaloweza kuonekana kuwa chungu na gumu kuchukuliana nalo litathibitika kuwa baraka. Pigo la kikatili linaloondoa raha hapa duniani litakuwa ni njia ya kuinua macho kuelekea mbinguni. Ni wangapi ambao kamwe wasingemjua Yesu kama huzuni isingewafanya wamtafute kwa ajili ya faraja?...
▶ Bwana atatenda kazi kwa ajili ya wale wote wanaoweka tegemeo lao kwake. Waaminifu watapata ushindi wa thamani kubwa. Mafundisho ya thamani yatajifunzwa. Uzoefu wa pekee utafahamika….
▶ Kristo huinua moyo wenye toba na kutakasa nafsi inayoomboleza hadi iwe makazi yake.
ubarikiwe
ReplyDelete